Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale akaliwa kooni, aandika waraka mzito

Babu Talexx 1080x640 Babu Tale

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Baada ya kutumia mfano wa wimbo wa Mario wa mama Amina, mbunge wa Morogoro Kusini, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ amejikuta akiandamwa na waja mitandaoni kuwa hakuwa na lengo zuri kuutaja wimbo huo. Tale alitumia mfano wa wimbo huo alipokuwa akijenga hoja kwamba Baraza la Sanaa la Taifa limekuwa likifungia nyimbo kwa ubaguzi, kuwafungia wale ambao wanataka kuwafungia lakini wengine wakiwaacha. Kufuatia maneno hayo ndipo watu wakamshukia mtandaoni kwa kumuambia aliutumia wimbo huo kama kumchongea Marioo afungiwe maana kiitikio chake kina tafsiri ya matusi. Katika kujitetea Tale aliandika waraka huu kwenye ukurasa wake wa Instagram: Unajua moja ya kazi kubwa ya mshumaa ni kuangaza na kuondoa giza lililotanda, lakini yuko mwingine anaweza kutafsiri kuwa unafanya ibada au ushirikina pale unapowasha mshumaa huo na asielewe maana ya mwanga anaouona.

Ukiitazama tasnia ya muziki kwa jicho la ushindani/ushabiki, unaweza kumlaumu kila anayesimama na kupigania maboresho ya paa linalovuja kwa kuwa wewe haujavujiwa na kuamini uko salama kumbe nyumba ni moja na paa ni hilohilo.

Kwanza natamani watu ambao wanaoujua muziki huu kwa kuusikia ndio waelewe zaidi kwa kuwa wanaoimba na kuandika huu muziki wanauelewa kwa kina tayari juu kila nilichomanisha, labda wajitie tu upofu. Unapokuwa Baba au Mwalimu huwezi kumchagua mtoto au mwanafunzi wa kumtolea mfano pale unapodhamiria kujenga uelewa wa kile unachokifundisha.

Kufundisha kwa mifano hakumaanishi kushitaki, kubeza wala kuumiza unayemtumia katika mfano, isipokuwa ni namna ya kulikoleza somo miongoni mwa wanaojifunza.

Sisi kama familia ya muziki tutatetea na kuipigania familia kutokana na tunayopitia, hatutotumia mifano iliyo nje ya familia. Hivyo tutamtaja yeyote aliyeko kwenye familia hii kama mfano ili somo lieleweke.

Zaidi ya yote, hitaji ni kwamba, tunataka ufanisi, maslahi, heshima na kutambuliwa kwenye hii tasnia ambayo tuna ushahidi wengine imetupandisha ngazi za kuaminiwa.

Hivyo UTETEZI usigeuzwe mtaji wa kutenganisha, kupotosha na kuunda migogoro ili kuwafanya wengine waone hawakuwa sehemu ya kutetewa bali kukandamizwa..."HAPANA"...msivuruge somo, tuko darasani na mifano itaendelea.

MUZIKI WETU, MAISHA YETU.

Chanzo: Tanzania
Related Articles: