Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yaweka tayari kikosi cha kijeshi kitakachofanya operesheni Niger

ECOWAS Yaweka Tayari Kikosi Cha Kijeshi Kitakachofanya Operesheni Niger ECOWAS yaweka tayari kikosi cha kijeshi kitakachofanya operesheni Niger

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS imeidhinisha hatua ya kijeshi kutumika nchini Niger dhidi ya viongozi wa kijeshi walioingia madarakani kwa kuipindua serikali ya Rais Mohamed Bazoum.

ECOWAS imesema inaweka tayari kikosi cha kijeshi kitakachofanya operesheni Niger ili kurejesha utawala unaotambulika kikatiba.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo amesema matumizi ya nguvu za kijeshi itakuwa njia ya mwisho.

Rais wa Ivory Coast Alassane Outarra amesema takriban wanajeshi elfu moja wa nchi yake watajiunga na kikosi hicho.

Wiki iliyopita, Senegal, Benin na Ivory Coast zilijitolea kupeleka wanajeshi iwapo jumuiya hiyo ya kikanda itaamua kuingilia kijeshi nchini Niger.

Kamishna wa ECOWAS wa Masuala ya Kisiasa, Usalama na Amani, Abdel -Fatau Musah aliambia BBC kwamba wanajeshi watatumwa wakati wowote.

"Hatutafanya mazungumzo milele. Operesheni hiyo itasitishwa tu ikiwa mamlaka ya kijeshi ya Niger litaamua kufanya mazungumzo ya kumrejesha madarakani Rais Bazoum na kuirejesha nchi kwenye utawala wa kikatiba,” Bwana Musah aliongeza.

Kamishna huyo pia alidokeza kuwa Rais Bazoum alikuwa akiishi chini ya "mazingira yasiyo ya kibinadamu" baada ya kukataa kwake kutia saini hati za kujiuzulu.

Jumuiya ya ECOWAS ilikariri kulaani mapinduzi na kuendelea kuzuiliwa kwa Rais Bazoum, ikisisitiza kuwa haitaomba msaada kutoka nje katika kushughulikia mzozo wa kisiasa wa Niger.

Chanzo: Bbc
Related Articles: