Ngoma ya #Cinderela ya kwake Alikiba (@officialalikiba ) ndio wimbo uliomtambulisha kwenye soko la #BongoFleva na kumfungulia milango ya safari yake kwenye muziki huo ila unaambiwa Alikiba mwenyewe hakuwa anaiamini ngoma hiyo kabisa bali alikuwa anataka wimbo wa #NakshiNakshi ndio utoke kwanza
Dusko Dalla ambaye alikuwa meneja wa G Records (Studio iliyofanya wimbo wa Cinderella) amepiga stori na @yoram004 na kueleza namna Alikiba alivyokuwa akipinga wimbo huo kutoka
"Alikuwa anasema #NakshiNakshi ndio wimbo pendwa nyumbani kwao lakini nikamwambia wimbo wa Cinderella ndio wimbo wa kumtoa na sababu kwa kipindi kile pale studio walikuwa wakiniamini sana ilibidi wakubali ndio Cinderella ikatoka na ukawa wimbo mkubwa"
"Watu hawajui kuwa Alikiba Alisota sana kabla ya kutoka na alikuwa amerekodi nyimbo nyingi pale G Records."