Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba: Sitofanya video ya 'Mahaba' licha ya kupendwa na Kamala

Alikiba Hnnnn Alikiba

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alikiba, Mflame wa muziki wa Bongo Fleva kwa mara ya kwanza amefunguka ni kwa nini anataka kuchukua mkondo wa kuacha kufanya video kwa ajili ya nyimbo zake mpya.

Kiba anahisi kwamba video zinamaliza pesa na mtaji wa wasanii wengi ambao wanajitahidi kuwekeza katika video za kupendeza lakini mapato yake huwa finyu sana ikilinganishwa na ‘audio’ tu.

Akihojiwa, staa huyo amesema ameanza kufanya video zilizopo na mishororo ya maneno anayoyaimba kwenye muziki yaani ‘lyrics video’ au kufanya video ya kucheza tu kama njia moja ya kukata hasara zinazotokana na kuwekeza katika video halisi ya ngoma ambayo mwisho wa siku huwa hairudishi faida kwa msanii.

“Ni kweli tunafanya video lakini ukweli video zinachukua pesa nyingi sana kwa wasanii, na wanasubiri pesa zirudi. Unajua muziki ni biashara, mimi nimejaribu kufanya mwaka huu lyrics video au hata dance video ili waone jinsi nilivyoimba muziki wangu kupitia huko,” Alikiba alisema.

Msanii huyo wa muda mrefu alisema kwamba amefanya utafiti huo baada ya kutoa video nyingi kwenye albamu yake ya The Only One King ambapo baadhi ya video ziliingiza pesa na zingine hazikurudisha faida hata moja.

“Wasanii wamekuwa wakipoteza pesa bila kujijua, huu utafiti nimeufanya baada ya kutoa The Only One King, kuna baadhi ya video ziliingiza pesa na zingine hazikuingiza pesa. Ukilinganisha na Audio ambazo zinachukua mizizi pakubwa na kuingiza kipato kikubwa bila kugharamika Zaidi,” Msanii huyo alidhibitisha.

Aliyasema haya wakati baadhi ya mashabiki wengi kuuliza watarajie video ya goma lake jipya la ‘Mahaba’ inatoka lini.

Audio huwa zinachukua mizizi pakubwa kutokana na majukwaa mengi ambayo ni pamoja na Boomplay, Spotify, Audiomac na nyingine lakini kwa upande wa Video, wengi hutegemea tu mtandao wa YouTube ambao wengi wamekuwa wakilalamika kuwa hauingizi hela za kutosha ikilinganishwa na majukwaa hayo ya audio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: