Wed, 2 Feb 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kwa kipindi cha kuanzia Januari 1, 2021 hadi Januari 31, 2022 matukio 176 ya mauaji yameripotiwa na watuhumiwa 150 wamekamatwa hadi sasa. Mikoa inayoongoza ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ametaja sababu za mauaji kuwa ni pamoja na kuwania mali, visasi, ushirikina, migogoro ya ardhi na wivu wa kimapenzi.
Wizara imeunda Kamati inayowashirikisha Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Wakili wa Serikali, Usalama wa Taifa, na Ustawi wa Jamii na itatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: