Mahakamani Kuu Kanda ya Iringa ambayo imefanya kikao mkoani Njombe imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Katekista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Makambako Daniel Philipo Mwelango mwenye umri wa miaka 43 kwa kosa la mauaji baada ya kukutwa na hatia.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 8, 2022 kwa kumuua Daniel Elias Myamba mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa mtaa wa Kahawa Makambako kesi Na MC 74/2022 katika mtaa wa Bwawani mjini Makamabako. Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. Said Kalunde.
Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.
Jaji Kalunde amesema siku ya tukio mshitakiwa alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga,Chuma pamoja na mifuko minne ya Kinga njaa,mifuko miwili ilikuwa kwa ajili ya kuzuia damu isisambe na miwili mingine kwa ajili kuhifadhi mwili wa marehemu.
Baada ya hapo akampiga na chuma kwenye kisogo baada ya kuona ameanguka chini na kufariki alimkata vipande viwili na kuvipaki katika mifuko ya kinganjaa ili iwe rahisi kubeba mwili huo na kwenda kuutupa mbali
Baada ya kuona mke wa marehemu anapiga simu mara kwa mara kwenye simu ya Maherehemu pamoja mwenyekiti wa kigango alishindwa kuubeba mwili huo na kuamua kuondoka huku akiwa amelibeba panga na kwenda kulitumbukiza katika shimo la choo cha shule ya msingi Makambako na chuma alichotumia kumpiga nacho alikificha kwenye gata karibu na duka na yeye kutorokea Dar es Saalam.