Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua kwa risasi 5 mtoto wake wa wiki moja kisa amezaliwa wa kike

Risasiiii Muuaji akiwa amekamatwa

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shahzaib Khan mwanaume wa nchini Pakistani ametiwa mbaroni na polisi kwa kutajwa kumuua mwanae wa kike mwenye umri wa wiki moja, amemuua kwa kumpiga risasi tano.

Sababu ya kumuua mtoto wake imeelezwa kuwa alitaka mtoto wake wa kwanza kuzaliwa awe wa kiume na sio wa kike kama ilivyotokea. Mtoto aliyeuawa alipewa jina la Jannat (Mbingu/pepo).

Shahzaib na mkewe wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili, baada ya mkewe kujifungua na kusikia kazaa mtoto wa kike, Shahzaib alisita kurudi nyumbani lakini baadaye alirudi na kuwakuta wanafamilia nyumbani.

Baada ya hapo, alimuomba mkewe amkabidhi mtoto ndipo akampiga risasi tano na kupoteza uhai na kukimbia, lakini hata hivyo alidakwa siku iliyofuata yaani Jumanne wiki hii.

Ndugu wa kiume upande wa mke amelaani kitendo hicho na kueleza kwamba walipotaka kumdhibiti alikuwa anawatishia na bastola.

Suala hilo limeibua hasira miongoni mwa Wapakistani wakitaka mume huyo achukuliwe hatua Kali za kisheria

Nchini Pakistani kwa miongo mingi baadhi ya makabila wanaamini kupata mtoto wa kike ni kama tusi kwa uanaume hivyo baadhi ya wanaharakati nchini humo kukemea imani hizo potofu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: