Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mpango ashiriki mdahalo Doha

MPANGO JK.jpeg Dkt. Mpango ashiriki mdahalo Doha

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameshiriki katika mjadala uliobeba ajenda ya uwekezaji kwa watu wote pasipo ubaguzi, ulioshirikisha Viongozi wakuu wa nchi na Serikali wanaoshiriki mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato cha chini unaofanyika Doha, Qatar.

Akichangia mada katika mjadala huo, Makamu wa Rais amesema katika kuwekeza kwa watu, Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuboresha miundombinu ya shule pamoja na ujenzi wa shule za wanawake maalum kwa masomo ya Sayansi kila mkoa.

Ameongeza kuwa ili kuendana na wakati wa sasa, Tanzania inafanya mabadiliko ya mitaala ya kufundishia pamoja na kujikita katika elimu ya TEHAMA kwa kutoa vifaa vya kidijitali kwa walimu ili waweze kufanikisha lengo hilo.

Makamu wa Rais amesema, ili kuhakikisha elimu inakua jumuishi bila ubaguzi, Tanzania imefanikiwa katika kuwarudisha masomoni wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kupata ujauzito.

Dkt. Mpango yupo nchini Qatar kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato cha chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: