Mamlaka ya Senegal imechukua uamuzi huo ikiwa ni katika mwendelezo wa kupunguza nguvu ya wapinzani, siku chache tangu kumweka kizuizini kiongozi wa upinzani.
Mgogoro wa kuwania madaraka kati ya kiongozi wa Chama cha Pastef, Ousmane Sonko na Rais Macky Sall umesababisha maandamano ya vurugu na kuharibu sifa ya Senegal kuwa moja ya Nchi yenye demokrasia thabiti Afrika Magharibi.
Senegal iliifuta Pastef na kuzuia upatikanaji wa huduma za intaneti Julai 31, 2023 huku Waziri wa mawasiliano alitumia uhalali sawa kuzuia TikTok.
Waziri Moussa Bocar Thiam amesema "Programu ya TikTok ni mtandao wa kijamii unaopendelewa na watu wenye nia mbaya ya kueneza jumbe za chuki na uasi."