Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabomu yaliyotegwa ardhini yasababisha kero kwa wananchi

MABOMU SD Mabomu yaliyotegwa ardhini yasababisha kero kwa wananchi

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dunia hivi leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha uondoaji wa mabomu ya kutegwa ardhini.Nchini Sudan Kusini, watu zaidi ya elfu 5 wameripotiwa kufa kutokana na milipuko ya kutegwa ardhini, huku mamia ya hekari ya ardhi yake ikitajwa kusheheni mabomu ya kutegwa.

Itta Betty Mogga raia wa Sudan Kusini aliyepata mafunzo kuhusu namna ua kuondoa mabomu ardhini anaelezea hali halisi katika nchi yake.

“Mabomu ya ardhini na vilipuzi ambayo yangali kwenye sehemu ambazo zilikumbwa na mapigano, ni hatari kwa usalama wa watu. Kdri tunavyopigana vita dhidi ya gonjwa hatari la korona, inabidi kuelewa kuwa kuna vitu ambavyo ni hatari jinsi hali ilivyo sasa,“ amesema Itta Betty Mogga raia wa Sudan Kusini.

Serikali inakiri kuwa, bado inaendelea kukabiliwa na changamoto kuondoa mabomu hayo kama anavyoeleza Jurkuch Barach Jurkuch, mwenyekiti wa shirika la taifa la Sudan Kusini linalohusika na uondoaji wa mabomu.

“Mabomu haya yalitegwa ardhini wakati wa vita lakini kwa sasa hakuna vita. Hata hivyo inafaa ikumbukwe kuwa mabomu yaliyoko ardhini hayana muda wa kuoza bali yanaweza kuwemo ardhini kwa miaka mingi, ili mradi tu hayachokozwi au kuchokorwa na mtu,“ ameeleza Jurkuch Barach Jurkuch, mwenyekiti wa shirika la taifa la Sudan Kusini linalohusika na uondoaji wa mabomu.

Tangu Sudan Kusini iwe nchi huru julai 2011 zaidi ya mabomu bilioni moja yaliyolenga binadamu, yameharibiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Naye, mkurugenzi wa shirika linalohusika na uondoaji wa mabomu Sudan Kusini, Francis William Ogrady, anasaema kuwa tangu mwaka 2006 zaidi ya mita bilioni moja mraba zimethibitishwa kuwa salama kutokana na kazi ya uondoaji wa mabomu. Mita milioni 16 mraba zingali haziandolewa mabomu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: