Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ni tete huko Niger

Niqer Hali Tete.jpeg Hali ni tete huko Niqer

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya wasiwasi imetanda katika nchi ya Niger huku muhula uliotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharfibi mwa Afrika (ECOWA) kwa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini humo kuachia madaraka na kurejesha utawala wa kikatiba ukimalizika leo, la sivyo watakiona cha mtema kuni.

Leo Jumapili, Agosti 6 ni siku ya mwisho ya muhula uliotolewa na ECOWAS kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger kukabidhi madaraka ya nchi kwa serikali iliyoondolewa madarakani.

Kamishna wa "ECOWAS", Abdul Fattah Moussa, amesema kwamba makamanda wa jeshi la kundi hilo wameandaa mpango wa uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger, ikiwa ni pamoja na namna na muda wa kutumwa kwa vikosi vya jeshi nchini humo.

Hata hivyo, chanzo cha kijeshi mjini Niamey kimeiambia televisheni ya Al-Jazeera kwamba, jeshi la Niger halitarudi nyuma katika hatua zake za kusimamisha katiba na kumpindua Rais Mohamed Bazoum.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa serikali iliyopinduliwa pamoja na serikali ya Rais Mohamed Bazoum ya Niger ametoa mwito wa kufanyika mazungumzo ili kuhitimisha mzozo huo.

Kuanzia Ijumaa iliyopita pia, Niger inashuhudia maandamano ya kuunga mkono viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini kote, huku bendera za Niger na Russia zikipeperushwa pamoja na picha za wanajeshi waliofanya mapinduzi hayo.

Maandamano ya kuunga mkono mapinduzi, Niger Abubakar Kimba Kolo, Mratibu wa Kamati ya Kusaidia Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi, amewataka wananchi kulinda maeneo yote ya kistratijia kwa lengo la "kufuatilia mienendo inayotia shaka", akisema kuwa operesheni hiyo ya wananchi ni sehemu ya "mapambano ya raia kuunga mkono mapinduzi."

Kwa upande wake, Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune ameonya dhidi ya kuingilia kijeshi nchini Niger, na kusema kwamba mashambulizi dhidi ya Niger ni tishio la moja kwa moja kwa Algeria.

Tebboune amesisitiza kuwa "mashambulizi ya kijeshi hayatatui lolote, kinyume chake, yatazidisha hali mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: