Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria: Hatuungi mkono uingiliaji wa kijeshi nchini Niger

Niqer Algeria.jpeg Algeria: Hatuungi mkono uingiliaji wa kijeshi nchini Niger

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Algeria imepinga vikali mpango wa kuingia kijeshi nchini Niger, kwa lengo la kuhitimisha mapinduzi ya kijeshi ya mwishoni mwa mwezi uliopita, yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ameiambia kanali ya Ennahar TV kwamba, uingiliaji wa kijeshi nchini Niger unaweza kuchochea moto wa vita katika eneo zima la Sahel barani Afrika, akisitiza kuwa Algiers kamwe haitatumia nguvu dhidi ya majirani zake.

Kauli ya Rais wa Algeria imetolewa baada ya wakuu wa kijeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kukubaliana na mpango wa kuingilia kijeshi Niger wakati muda waliowapa wanajeshi waliofanya mapinduzi utakapomalizika.

Wakati huohuo, serikali ya Ufaransa imekataa miito ya kutakiwa iwaondoe wanajeshi wake Niger ikisisitiza kuwa, inaunga mkono mashinikizo ya nchi za Afrika Magharibi za kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum aliyepunduliwa.

Hii ni licha ya maelfu ya wananchi wa Niger hivi karibuni kufanya maandamano katika mji mkuu Niamey, wakitaka kufukuzwa nchini humo mara moja wanajeshi wa Marekani na Ufaransa.

GĂ©rard Araud, balozi wa zamani wa Ufaransa nchini Marekani, Umoja wa Mataifa na katika utawala haramu wa Israel amesema mapinduzi ya kijeshi Niger yanatokana na wananchi kuchoshwa na uingiliaji wa Ufaransa na kukataa kwao uwepo wa dola hilo la Ulaya nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: