Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Patrick: Haya ni matokeo ya ushabiki wa wachambuzi

Wakili Pat Wakili Patrick: Haya ni matokeo ya ushabiki wa wachambuzi

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu sakata la Kibu Denis kuwazimia simu viongozi wa Simba na kutimkia nchini Norway.

"Hizi changamoto za wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao ni matokeo ya ushabiki na wachambuzi wetu.

"Kwa sasa, kuna wimbi la wachezaji kutoroka na wengine kuwa na mikataba na timu zaidi ya moja kwa madai kwamba hawana furaha na wanaenda kutafuta fursa bora zaidi.

"Ushauri wangu kwa BMT ili kuokoa soka letu ni kuweka kanuni inayolazimisha mchezaji yeyote mwenye mkataba akihama kutoka klabu moja kwenda nyingine lazima kuwe na Mkataba wa Uhamisho (Transfer Agreement) au Mkataba wa Kusitisha kwa Pamoja (Mutual Termination Agreement) uliothibitishwa na BMT na kulipiwa ushuru wa stampu (Stamp Duty).

"Mchezaji au timu yoyote ikikiuka, basi mchezaji huyo asipewe kibali cha kucheza nchini, period.

"Bila hatua hiyo, migogoro ya wachezaji wenye mikataba haitaisha kamwe na TFF itaendelea kulalamikiwa bure.

"NB: Kwakuwa tulishakubaliana kama mchezaji hana furaha aruhusiwe kuondoka, Rasta asiguswe acha ale maisha," amesema Wakili Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: