Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yarejea kwa Mpanzu kama mbadala wa Kibu

Mpanzu Simba yarejea kwa Mpanzu kama mbadala wa Kibu

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba SC imelirejesha mezani jina la winga, Elie Mpanzu Kibisawala raia wa Congo DR na wametuma ofa ya USD $200,000 kwa AS Vita Club kwa ajili ya kumsajili.

Huku hali ya Kibu ikiwa haijaeleweka, Simba inapambana kuona uwezekano wa kumleta Mpanzu Tanzania ambapo hapo awali walionesha nia ya kumtaka lakini baadaye wakapiga chini dili hilo.

Vita Club bado wanashikilia shilingi wakitaka wapewe dola $250,000 kabla ya kumruhusu nyota wao kuondoka.

Simba imekuwa wazi kila wakati wakisema Mpanzu ndiye anayelengwa katika dirisha hili la usajili japo hapo awali Vita hawakuwa tayari kumwachia.

Nafasi ya Kibu ndani ya Simba inazidi kupungua, baada ya kutoroka kwenye timu hiyo na kutimkia nchini Norway ambako anadaiwa kupata dili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: