Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Museveni kutunukiwa tuzo ya Uviko-19

Uviko 19 Museveni Rais Museveni kutunukiwa tuzo ya Uviko-19

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anatarajiwa kupokea tuzo ya kimataifa kwa namna alivyojitoa katika mapambano dhidi ya Uviko-19 katika nchi yake.

Museven atapokea tuzo hiyo Julai katika mkutano wa kwanza wa kimataifa baada ya Uviko-19 unaotarajiwa kufanyika katika Mji wa Toronto nchini Canada.

Mkutano huo wa kimataifa umeandaliwa na Shirika la Livelihood Development Initiatives International (LDII) Canada, kwa ushirikiano na Serikali ya Canada, Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (Igad), Umoja wa Afrika Kanda ya Sita Duniani, Shirika la Afya Duniani (WHO), Continental Investments LLC. -Vietnam na Umoja wa Mataifa.

Mbali na Rais Museveni baadhi ya viongozi wengine wa Uganda wanaotarajiwa kutambuliwa ni Waziri wa Afya Jane Ruth Aceng, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Monica Musenero, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Diana Atwine, makamu wa Rais wa zamani, Specioza Kazibwe, na mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Virusi Uganda Profesa Pontiano Kaleebu.

Pia, inaelezwa kuwa watu takribani 11 ambao ni maofisa wa Serikali, wanasayansi na wafanyabiashara watatambuliwa kutokana na namna walivyopambana katika kudhibiti Uviko-19 katika maeneo mbalimbali duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: