Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Taarifa ya Simba ni ya kiubabaishaji

Edo X Kibuuuuu Edo Kumwembe: Taarifa ya Simba ni ya kiubabaishaji

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Nilisikia minongono kwamba huenda Kibu amepata timu barani Ulaya. Vyovyote ilivyo atakuwa amepishana na gari la mshahara. Ingekuwa hajasaini Simba, basi ingekuwa rahisi kuondoka zake kama mchezaji huru. Lakini sasa Simba wana mkataba wake.

Simba ndio ambayo inaweza kuamua kumuuza au vinginevyo. Hana tena nafasi ya kuondoka kama mchezaji huru. Huwa inatokea. Ni kama ilivyowatokea Coastal Union kwa Lameck Lawi. Walipomuuza kwenda Simba tu ndipo ikatokea timu kutoka Ubelgiji. Nadhani ndio maana walirudisha pesa za Simba.

Kuna mambo mawili ambayo inabidi tujifunze katika mpira wetu. Maisha ya mchezaji na klabu. Simba walipaswa kulitolea ufafanuzi suala la Kibu kwa muda mrefu. Kama haufanyi hivyo ni wazi kwamba unawayumbisha mashabiki. Mashabiki wana haki ya kupewa taarifa kuhusu wachezaji wao. Hata kama taarifa yenyewe ni fupi na inayojaribu kuficha mambo mengi. Kule kwa wenzetu huwa tunaona taarifa mbalimbali zinazohusu kukosekana kwa wachezaji. Iwe kwa majeraha, iwe kwa kadi za uwanjani au matatizo ya kifamilia.”. — Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: