Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Makamba: Maneno yanatusaidia yaendelee

Bwawa Pic Makamba Januari Waziri Makamba

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, January Makamba jana Ijumaa, Juni 1, 2023 alihitimisha Mjadala wa Makadirio ya mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara ya Nishati Bungeni jijini Dodoma.

Miongoni mwa aliyoyazungumza Waziri Makamba ni kuhusu yale yaliyokuwa yakiendelea mitandaoni.

“Haya maneno yanatuongezea hamu na hamasa ya kupata matokeo. Sisi hamasa yetu ni imani ya Mheshimiwa Rais kwetu, hamasa yetu ni matokeo ya kazi yetu kwa uhai wa chama chetu.

“Hamasa nyingine ni kuwasaidia Watanzania kwa majukumu tuliyopewa. Lakini hamasa ya mwisho ni maneno haya, mtu akikusema wewe hufai maana yake unajitahidi ili uonekane unafaa. Kwa hiyo haya maneno yanatusaidia.

“Lakini pia haya maneno yanatusaidia kwa sababu yanawaamsha wanaotupenda na wanaotutakia heri ili watuombee dua na sala.

“Maneno haya yanatusaidia kwa sababu yanatufundisha ukomavu, yanatufundisha kuwa na subra, yanatufundisha kuwa na uvumilivu na yanatujenga kuwa viongozi bora zaidi.

“Sisi tumesema waendelee kwa sababu yanatusaidi. Sisi kisasi chetu ni MATOKEO. Hatutabishana, hatutatupa maneno, hatutajitetea, tutalipa kisasi kwa matokeo,” amesema Makamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: