Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua na kuridhia uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:
Amemteua Bw. Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority – TFRA). Kabla ya uteuzi Bw. Laurent alikuwa Mhadhiri, Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania).
Ameridhia uteuzi wa Bw. Patrick Magologozi Mongella kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board – CPB). Bw. Mongella ni Mkurugenzi wa Miradi, Benki ya Maendeleo TIB.
Ameridhia uteuzi wa Bi. Mwanahiba Mohamed Mzee kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Trust Fund – AGITF). Bi. Mwanahiba aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.
Ameridhia uteuzi wa Bi. Irene Madeje Mlola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Regulatory Authority – COPRA). Bi Mlola aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Financial Sector Deepening Trust (FSDT).
Ameridhia uteuzi wa Dkt. Andrew Marcelin Komba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Authority – NFRA). Bw. Komba ni Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais.
Ameridhia uteuzi wa Bw. Felix H. Mlaki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Limited – NARCO). Bw. Mlaki ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya NARCO.