Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia na Hichilema wawakumbuka mashujaa

Samia Hicilemaa.jpeg Rais Samia na Hichilema wawakumbuka mashujaa

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, leo Jumanne Juni 24, 2023, wameongoza mamia ya wananchi wa Zambia katika dua na kuweka mashada ya maua kwenye mnara wa mashujaa uliopo la mtaa wa Uhuru Lusaka, Zambia.

Pamoja na mnara huo wa mashujaa pia Rais Samia aliweka mashada ya maua katika kaburi la muasisi na baba wa Taifa hilo, Kenneth Kaunda.

Aidha, viongozi wa dini, mabalozi, ndugu wa mashujaa waliopoteza maisha na viongozi wa Kitaifa wa Taifa hilo waliweka mashada katika mnara huo.

Katika tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa Kitaifa wa nchi hizo mbili na wananchi, jambo kubwa lililosisitiziwa ni kudumisha amani na ushirikino wa kidugu baina ya nchi hizo.

Shughuli hiyo imeongozwa na Jeshi la Zambia kwa maandamano ya gwaride na vikundi vya asili vya akinamama.

Awali, Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema alianza kuwasili eneo Kamwala jijini Lusaka majira ya saa 8:50 saa za Zambia na kumpokea mgeni wake Rais Samia Suluhu Hassan aliyewasili hapo saa 9:02.

Shughuli hiyo imeambatana na sherehe za miaka 59 ya Uhuru Zambia yenye kauli mbiu Kuharakisha maendeleo ya Taifa kupitia rasilimali zilizopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: