Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kufungua Mkutano Maafisa wa Polisi

Rais Samia Uapisho Rais Samia kufungua Mkutano Maafisa wa Polisi

Sat, 2 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maafisa Wakuu Waandamizi kutoka Makao Makuu, Mikoa na Vikosi kuanzia Septemba 4, 20223 jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akitoa taarifa hiyo hii leo Septemba 2, 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema, katika mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalam kutoka vyuo vya hapa Nchini na wataalam wa kada mbalimbali ambapo amesema maafisa washiriki watapata fursa ya kufanya tathmini ya majukum ya Jeshi la Polisi na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa mwaka 2022 na Rais Samia.

Misime pia ameongeza kuwa, Mikutano hiyo ni utaratibu uliowekwa na Jeshi la Polisi ili kuwakutanisha maafisa wakuu waandamizi Pamoja kufanya tathmini na kuweka mikakati ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa Nchini na utaongozwa na kauli mbiu isemayo matumizi ya Tehama kuleta uwazi na ufanisi katika utendaji wa Jeshi la Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: