Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awataka vijana kutumia vizuri mitandao ya kijamii

Samia Nyieee Rais Samia Suluhu Hassan

Sun, 14 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 13 Mei, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwani kuna uhuru wa kusema, kutafuta jambo au habari kwani simu inakuwa mkononi mwako kwa hivyo kufanya unalotaka.

Rais Samia ameendelea kuwataka vijana watumie mitandao ya kijamii kwa maendeleo zaidi kwani ina manufaa yake na siyo vinginevyo.

Rais Samia ameyasema hayo jana Mei 13, 2023 aliposhiriki hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya Simu katika kata 763 nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: