Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awapa machinga kiwanja na Tsh milioni 10

Samia Road.jpeg Rais Samia Suluhu Hassan

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Umoja wa Machinga wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekabidhiwa kiwanja chenye hatimiliki pamoja na Tsh milioni 10 ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yao.

Akizungumza Katibu Mkuu wa shirika hilo, Venatus Magayane amesema kila Mkoa wenye wafanyabiashara hao, Rais Samia amewapa Tsh milioni 10 na kiwanja chenye hatimiliki kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, hivyo baada ya ujenzi kukamilika machinga watakuwa na nafasi ya kukopesheka na tassisi za kifedha tofauti na hapo awali.

Amesema kwa sasa wameridhishwa na lengo la Serikali chini ya Rais Samia katika kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Mmoja wa Machinga, Agnes Magoli amesema mara ofisi zitakapokamilika zitawasaidia kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao watakuwa wakichangia kodi Serikalini kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Aidha, kwa kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa Machinga hao, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amewaongezea Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: