Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aunda Kamati kuchunguza Polisi, Takukuru, Magereza

Samia Oman LEO.png Rais Samia Suluhu Hassan

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema ameunda kamati maalum ambayo itakuwa na jukumu la kuchunguza na kumshauri namna bora ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora katika vyombo vya haki jinai.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 20, 2022 katika hafla ya kuwaapisha viongozi wateule akiwemo IGP Camillius Wambura iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Nimeunda kamati ya watu 12 na sekretarieti ya watu watano. ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande Othumani Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti atakuwa mstaafu Balozi Ombeni Sefue,” alisema Rais Samia.

Rais Samia amesema ameunda kamati hiyo ili kuangalia miundo iliyopo kwenye vyombo hivyo kama inakidhi mahitaji yaliyopo ili kama haiendani basi maboresho yafanyike ambapo wataanza na Polisi kisha itafuata Ofisi ya Mashtaka (DCI), Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Magereza.

Amesema, anafahamu kwenye majeshi hayo kunahitaji maboresho katika fani mbalimbali kama vile teknolojia ya habari na fani nyingine ili kuleta ufanisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: