Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aridhia kufuta tozo za miamala ya simu

RAIS SAMIA KILIMO Rais Samia aridhia kufuta tozo za miamala ya simu

Tue, 4 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano chini ya Waziri Nape Moses Nnauye ya kufuta tozo katika miamala ya simu.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Injinia Kundo Mathew amesema hayo leo July 04,2023 akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Rukwa.

"Fahari ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais ni pamoja na kuwasikiliza Watanzania na Wananchi anaowaongoza, ndio maana ameruhusu na kutoa maelekezo ya moja kwa moja kuondoa tozo katika miamala ya simu"

"Rais wenu kipenzi Mkuu wa Nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu.

"Kila Mtu kwenye Familia yake ajue kwamba kuondoka kwa tozo hii ambayo ulitakiwa ukatwe labda Tsh.Elfu 5 haujanunua mboga jaman?, ni Rais mmoja tu ambaye ameona uchungu wa Watu wake na sisi tumuunge mkono," amesema Naibu Waziri Injinia Kundo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: