Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia alia na nidhamu Jeshi la Polisi

Rais Samia Suluhu Leo Mei 13 Rais Samia alia na nidhamu Jeshi la Polisi

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na tabia ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP) ‘kukaza buti’ Jeshi linyooke.

Akizungumza wakati wa Hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, Rais Samia amesema inasikitisha kuona bado kuna tatizo la nidhamu katika jeshi la polisi.

“Kuna kesi tunapokea, zingine tunaona katika mitandao mtu akipotoka. Bado kazi ipo ila ni kiri kuwa kidogo kidogo mabadiliko yataendelea kuwepo kutokana na mafunzo wanayoyapata,” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: