Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aendeleza kazi angani, India wampokea kwa kishindo

Samia 75751640 Rais Samia aendeleza kazi angani, India wampokea kwa kishindo

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini New Delhi, India jana Oktoba 8, 2023 kwa ajili ya kuanza ziara ya Kitaifa ya siku nne nchini humo.

Mapokezi rasmi ya Rais Dkt. Samia yatafanyika Oktoba 9, 2023 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa India, Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi.

Ziara ya Rais Dkt. Samia nchini India ni mwendelezo wa ushirikiano na uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo sekta muhimu nchini kama Afya, teknolojia, kilimo, uchumi wa buluu, biashara, uwekezaji, maji na elimu zinatarajiwa kuwa kipaumbele wakati wa majadiliano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: