Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Mungu kanipa mtihani

Magwanda Magwanda Samia Rais Samia Suluhu Hassan

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa nafasi aliyopewa, Mwenyezi Mungu amempa mtihani si haba.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 - Hijiria.

“Mungu kanipa mtihani si haba, pale aliponiweka, na ukisikiliza ya watu Samia Suluhu yule mmm…mtihani si haba nilio nao, nijiusie nafsi yangu kwanza, na niwausie na wengine, wote tushiriki na wote tuige mifano mizuri tunayooneshwa na viongozi wa dini hasa kutumia njia bora na hekima katika kuendesha maisha yetu.

“Tulioshika madaraka tuwe thabiti, tuwe na hekima katika kutoa maamuzi, sio unapewa dhamana husikilizi wengine, mtu anakuja na shida zake fulani msikilize huyo, kuweni wastarabu, sio kuweka mabega juu kama mizani ukipewa madaraka wanaume koti zinaninginia, wanawake shungi zipo sivyo,” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: