Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Hakuna mmiliki wa Tanzania

Samia Rais Samia.jpeg Rais Samia: Hakuna mmiliki wa Tanzania

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Nchi ya Tanzania haina mmiliki mmoja na kwamba ni nchi ya Watanzania wote.

Ameyasema hayo leo Septemba 11, 2023 kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

"Hakuna mtu aliyepewa waraka, au hati kwamba wewe ndio mmiliki wa Tanzania, hakuna.

Tanzania ni yetu sote. Hata kitoto kinachozaliwa leo kina share [sehemu] yake ndani ya Tanzania hii. Kwa hivyo hakuna mtu wa kujitokeza na kujifanya yeye ndio Mtanzania sana kuliko wengine."- Amesema Dkt Samia Suluhu Hassan

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: