Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msigwa: Waliotajwa ripoti ya CAG watashughulikiwa

Gerson Msigwaaa.jpeg Gerson msigwa

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amewataka Watanzania kutokuwa na hofu, kwani wote waliotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) watachukuliwa hatua.

Ripoti ya CAG yam waka 2021/22 ilikabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan Machi 29 ikulu ya Dar es Salaam na Aprili 6 ilikabidhiwa bungeni jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano, Aprili 19, 2023, Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, amesema yoyote aliyetajwa katika ripoti hiyo atachukuliwa hatua na wananchi wasiwe na wasiwasi.

"Nipo hapa kuwatoa hofu Watanzania niwahakikishie ripoti ya CAG inafanyiwa kazi na Watanzania wasiwe na wasiwasi na kila kitu kitakuwa sawa, wale wote waliotajwa katika ripoti hiyo watashughulikiwa," amesema Msigwa.

Kuhusu kuanza kazi kwa treni ya kisasa ya Mwendokasi (SGR) Msigwa amesema ilikuwa ianze Februari mwaka huu lakini wamesogeza mbele hadi Aprili mwishoni au mwanzoni mwa Mei kutokana na mkandarasi kutaka ijengwe fensi katika baadhi ya maeneo.

"Sababu ya kuchelewa wadau wametaka ijengwe fensi ya umeme, hii ni mara yetu ya kwanza kuna vitu bado tunajifunza," amesema Msigwa.

Katika hatua nyingine, Msigwa amesema siku ya uhuru wa vyombo vya habari inatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Mei 1-3 mwaka huu. Amesema katika mkutano huo watajadili mustakabali wa Waandishi wa Habari nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: