Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Msemaji Mkuu mpya wa Serikali Tanzania – Mobhare Matinyi

Mobhare Matinyi  Mobhare Matinyi.

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Julai 2 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Mwanahabari Mobhare Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Miezi mitatu baadaye amemteua Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Matinyi mbali na kuwahi kuwa mkufunzi katika Kituo cha Diplomasia cha Musumbiji-Tanzania amekuwa mwanahabari na mchambuzi wa maswala mbalimbali mengi yakilenga kuitetea Tanzania. Pia amewahi kuwa na ukurasa – column katika gazeti la kiingereza la ‘The Citizen’ – The Eagle’s Eye na ameandika Makala mbalimbali kupitia gazeti la Jamhuri.

Wengi wanamkumbuka Matinyi kwa uchambuzi wake tunduizi wa mabendekezo ya Chadema kuhusu Katiba mpya wakati huo akiwa kama Mshauri Mwelekezi huko nchini Marekani.

Hata hivyo, kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC. Kwa sasa Matinyi anaenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: