Madereva wa wasio na uzoefu wa magari ya familia katika safari ndefu wametajwa kuwa ni chanzo cha ajali za Barabarani zinazopelekea vifo au majeruhi nchini.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo wakati akitoa taarifa ya ajali iliyosababisha Watu watatu kupoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo, Pwani.
Amesema, ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba za usajili T478 DCQ iliyokuwa ikitoea Iringa kwenda Dar es Salaam iliyokuwa imebeba watu 7 wa familia moja kugongana na gari lenye namba za usaili T851 AQC aina ya Scania.
Katika ajali hiyo, iliyotokeamajira ya usiku wa Oktoba 23, 2023 watu wanne walijeruhiwa ambapo Kamanda lutumo amewataja kuwa ni Amina Kondo miaka 77 na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally.