Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu mabadiliko ya Wizara alizounda Rais Samia

Uteuzi Tena! Rais Samia Ateua Viongozi Wapya Fahamu mabadiliko ya Wizara alizounda Rais Samia

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi wa viongozi kama ifuatavyo;

Ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji ambapo amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Mkumbo alikuwa ni Mbunge wa jimbo la Ubungo.

Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Fedha,Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango.

Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo, Kabla ya Uteuzi huu Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Amemteua Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, Kabla ya Uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango(Usimamizi wa Uchumi).

Amemteua Bw. Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha(Usimamizi wa Uchumi), Kabla ya uteuzi huu Bw. Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: