Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Kijaji ateuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara

Kijaji 2 Ashatu Viwanda Dkt. Ashatu Kijaji.

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara ambapo ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara na amemteua aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Itakumbukwa Dkt. Kijaji alikuwa ni Waziri anayeshughulikia Viwanda, Biashara na Uwekezaji lakini kutokana na kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais sasa anabaki kuwa Waziri anayesimamia Viwanda na Biashara pekee huku Uwekezaji ukiunganishwa na Mipango na Waziri wake ni Prof. Kitila Mkumbo ambaye ameteuliwa na Rais Samia hii leo.

Rais Samia amemteua pia Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, kabla ya uteuzi huu Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).

Rais Samia amemteua pia Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi), kabla ya uteuzi huu Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: