Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Rais Samia amng'oa Sirro, ateua IGP mpya

Igp Sirro Samia Wambura Rais Samia ateua IGP mpya, amng'oa Sirro

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura na Kumteua kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Kupita taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Uteuzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Julai 20, 2022 ambapo kabla ya kuteuliwa alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI).

Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe.

Wakati huo huo amempadisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamis Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI).

Uteuzi mwingine ni kama ifuatavyo:



Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: