Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa akatwa kichwa kwa kukataa kuolewa

BINTI Auawaaaaa Binti wa akatwa kichwa kwa kukataa kuolewa

Fri, 25 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA nchini Pakistan imemuhukumu adhabu ya kifo mwanaume mmoja kwa kosa la kumbaka na kumuua binti wa mwanadiplomasia wa zamani, ambaye alikataa ombi lake la kuolewa.

Noor Muqaddam, aliyekuwa na umri wa miaka 27, alipigwa, kubakwa na kukatwa kichwa na Zahir Jaffer, ambaye ni mtoto wa miongoni mwa familia tajiri zaidi nchini Pakistan.

Mauaji hayo ya kikatili yalifanyika nyumbani kwake tarehe 20 Julai mwaka jana. Picha za CCTV zilimuonesha akijaribu kutoroka bila mafanikio.

Mauaji hayo yalizua taharuki nchini kote na kusababisha madai ya kutaka jitihada zaidi kufanywa ili kuhakikisha usalama wa wanawake unakuepo.

Mauaji ya Noor Muqaddam na mwanaume huyo aliyemfahamu katika kundi moja la marafiki wa jamii ya kitajiri yalikuwa yametawala vichwa vya habari kwa miezi kadhaa.

Ilileta wito wa kufanyiwa marekebisho mfumo wa haki ya jinai wa Pakistan, ambao una viwango vya chini sana vya hatia, hasa kwa uhalifu dhidi ya wanawake.

Mamia ya wanawake huuawa nchini humo kila mwaka, na maelfu huteswa huku kesi nyingi zikiwa haziripotiwi.

Jaffer alimteka Noor Muqaddam kwa muda wa siku mbili katika nyumba ya familia yake katika wilaya ya kifahari ya mji mkuu baada ya kukataa kuolewa naye.

Katika kusikiliza kesi hiyo, akizungumza na polisi mbele ya wanahabari nje ya mahakama, Jaffer alikiri kuwa alimuua... "Nilikuwa na hasira, nilimuua Noor kwa kisu."

Wafanyikazi wawili wa nyumbani kwa Jaffer walihukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa kusaidia mauaji hayo, huku wazazi wake waliachiliwa kwa kujaribu kuficha ukweli wa kilichotokea.

Baba yake, Shaukat Muqaddam, alisema uamuzi huo kuwa ni ushindi wa haki na akasema anataka kuhakikisha wanyanyasaji na wauaji wa wanawake nchini Pakistani hawakimbii uhalifu wao tena.

"Nina furaha kwamba haki imetendeka. Nimekuwa nikisema kwamba hii sio kesi ya binti yangu tu, ni kesi ya mabinti wote wa nchi yangu," alisema.

Aliahidi kupinga kuachiliwa kwa wazazi wa Jaffer. Jaffer, mwenye umri wa miaka 30 raia wa Marekani mwenye asili ya Pakistan, pia anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: