Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi Kairuki ahamishiwa Uingereza, Khamis Omar apelekwa China

Mbelwa Kairuki.jpeg Balozi Mbwela Brighton Kairuki.

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia amemhamisha Balozi Mbwela Brighton Kairuki kwenda London ambako anachukua nafasi ya Dkt. Asha Rose Migiro ambaye amemaliza Mkataba wake

Balozi Ceaser Chacha Waitara anakwenda Ubalozi wa Tanzania Nchini Namibia akichukua nafasi ya Balozi Modestus Kipilimba aliyestaafu. Kipilimba aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) (2016-2019)

Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse anakwenda Ubalozi wa Tanzania Nchini Kenya, anachukua nafasi ya Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene aliyehamishiwa Kampala, Uganda

Ikumbukwe, mabadiliko haya yanakuja muda mfupi baada ya kauli ya Rais Samia kuwa alipata malalamiko kutoka kwa Rais mmojawapo katika Nchi za SADC kuwa kuna Balozi wa Tanzania hawajibiki katika majukumu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: