Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Thiem atwaa Grand Slam ya kwanza hiem atwaa Grand Slam ya kwanza

Thiem Thiem atwaa Grand Slam ya kwanza hiem atwaa Grand Slam ya kwanza

Tue, 15 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

DOMINIC Thiem wa Austria, ametwaa taji lake la kwanza la Grand Slam, baada ya kupambana akiwa nyuma kwa seti mbili na kuibuka mshindi dhidi ya Alexander Zverev katika fainali za tenisi za US Open juzi.

Mchezaji huyo namba mbili duniani mwenye umri wa miaka 27, alipoteza fainali zake tatu kubwa zilizopita na ilionekana kama angepoteza ya nne pia juzi.

Lakini mchezaji mwenye umri wa miaka 23 Zverev akicheza fainali zake za kwanza za Slam, alijikuta akiharibu baada ya seti ya pili na Thiem kutumia nafasi hiyo kumuadhibu.

Wote wawili walishindwa kusevu vizuri kabla Thiem hajapata ushindi kwa 2-6 4-6 6-4 6-3 7-6 (8-6). “Natamani tungekuwa na washindi wawili leo (juzi), wote tulistahili,” Thiem alimwambia Zverev ambaye wamekuwa wakifahamiana tangu utotoni mwao.

Thiem ni mchezaji wa kwanza kushinda taji la Grand Slam kutoka nyuma kwa seti mbili tangu alipofanya hivyo Muargentina Gaston Gaudio kwenye French Open mwaka 2004.

Thiem, ambaye anabaki nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora duniani, anakuwa mwanaume wa kwanza kushinda taji la Grand Slam mchezaji mmoja mmoja tangu Mcroatia, Marin Cilic, alipofanya hivyo kwenye US Open ya mwaka 2014.

Kutokuwepo kwa bingwa wa mwaka 2019, Rafael Nadal na Mswisi Roger Federer, katika michuano hiyo iliyochezwa bila mashabiki, pamoja na kuondolewa mchezaji namba moja Novak Djokovic kwa kumpiga mwamuzi na mpira, kumefungua milango kwa majina mapya kuchomoza kwenye mataji makubwa.

Thiem anakuwa wa kwanza nje ya tatu bora kushinda taji la Australian Open, French Open, Wimbledon au US Open na kuwa bingwa tangu Mswisi, Stan Wawrinka, alipofanya hivyo Flushing Meadows mwaka 2016

Chanzo: habarileo.co.tz