Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Serena azungumzia Australian Open

C3f92951526759d39f7b6153a0971490 Serena azungumzia Australian Open

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERENA Williams amesema asingeshiriki michuano ya tenisi ya Australian Open kama isingesogezwa mbele kwa wiki tatu.

Michuano hiyo ya Grand Slam ya kwanza kwa mwaka huu imechelewa kuanza kutokana na kuruhusu wachezaji kujiweka karantini ya corona. Williams anataka kuwania rekodi ya kutwaa taji la 24 kwa mchezaji mmoja mmoja katika michuano hiyo iliyopangwa kuanza wiki ijayo.

Alisema alihitaji muda ili apone vizuri mguu wake alioumia kwenye US Open Septemba mwaka jana. Serena na Muingereza, Katie Boulter juzi walishinda mechi zao katika michuano ya maandalizi kabla ya Australian Open.

Wawili hao wanacheza michuano ya Gippsland Trophy moja kati ya matukio sita yanayofanyika Melbourne Park wiki hii kuruhusu wachezaji kufanya maandalizi kwa ajili ya Australian Open.

Boulter anacheza kwa mara ya pili michuano mikubwa ya WTA tangu Februari 2019, alimfunga mrusi, Anna Kalinskaya kwa 6-1 6-3. Williams pia aliibuka na ushindi wa 6-1 6-4 dhdi ya Daria Gavrilova wa Australia.

"Sidhani kama ningekuwa hapa kama ra- tiba ingeenda kama kawaida,” alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 na kuongeza: "Maumivu niliyopata yalikuwa makubwa sana, sikutarajia kama yangechukua muda mrefu kupona,” alisema.

Mchezaji huyo namba tano duniani atacheza na Tsvetana Pironkova wa Bulgaria katika hatua ya 16.

Chanzo: habarileo.co.tz