Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Serena atinga fainali US Open

16211 Pic+serena TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

New York, Marekani. Hatimaye Serena Williams amekaribia kulitwaa taji la US Open kwa mara ya sita na 24 la Grand Slam, baada ya jana kumchapa Anastasija Sevastova katika nusu fainali na kutinga fainali.

Wawili hao walichuana kwenye viwanja vya Flushing Meadows, mjini New York, ambapo Serena alitumia dakika 66 kushinda kwa seti mbili za 6-3 6-0 dhidi ya mchezaji huyo anyeshikilia nafasi ya 19 kwa ubora duniani.

Iwapo atafanikiwa kutwaa taji la US Open, litakuwa taji la kwanza kwa Serena tangu ajifungue kifungua mimba wake Olympia, aliyezaliwa Septemba mwaka jana.

Serena,36, aliyeshindwa na Angelique Kerber katika fainali ya Wimbledon, Julai mwaka huu, amefika fainali ya 31 ya Grand Slam na kesho Jumamosi atachuana na Naomi Osaka wa Japan katika fainali, kusaka taji la US Open.

Nyota huyo atakuwa akisaka taji lake la 24 la Grand Slam, akilingana na Margaret Court wa Ufaransa anayeshikilia rekodi ya kutwaa mataji mengi ya Grand Slam kwa wanawake duniani.

"Bila shaka fainali hii ya mwaka huu itakuwa na umuhimu sana kwangu kwani mwaka jana sikushiriki mashindano ya US Open, kwani nilikuwa nikipigania roho yangu katika uzazi wa mwanagu Olympia,” alisema Serena.

Alisema anajisikia vizuri na mwili wake upo vizuri akisubiri muda ufike ili aweze kulisaka taji hilo analolihitaji sana na kwamba anamheshimu Osaka kutokana na kiwango chake bora lakini anaamini atamshinda.

Chanzo: mwananchi.co.tz