Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Serena Willams aangushwa na msichana mdogo US Open

74758 Serena+pic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

New York, Marekani. Mchezaji mdogo wa tennis, Bianca Andreescu amekuwa raia wa kwanza wa Canada kutwaa ubingwa wa michuano mikubwa ya mchezo huo, Grand Slam baada ya kupata ushindi katika seti mbili (6-3, 7-5) dhidi ya Serena Williams, ambaye amneshatwaa mataji 23, katika fainali ya michuano ya US Open jana Jumamosi.

Mcanada huyo mwenye umri wa miaka 19 pia amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo kuwahi kutwaa ubingwa wa Grand Slam tangu Svetlana Kuznetsova atwae kombe la US Open mwaka 2004, baada ya kumpa Williams kipigo cha nne mfululizo katika fainali ya mashindano makubwa na kumzuia kufikia rekodi ya kutwaa mataji 24.

"Ni vigumu kueleza kwa maneno lakini nina furaha na kujisikia kubarikiwa. Nimefanya kazi kubwa, kubwa sana kwa ajili ya kufikia hapa," alisema Andreescu, ambaye alikuwa ameshinda mechi mbili tu kabla ya kucheza mechi ya kwanza ya US Open mwaka huu.

Aliporesha rekodi yake ya kuibuka na ushindi dhidi ya wachezaji 10 bora msimu huu hadi kufikia ushindi wa 8-0 na leo atapanda katika chati ya wachezaji bora duniani hadi kufikia nafasi ya tano leo.

"Mwaka huu umekuwa ni wa kutimia kwa ndoto. Kuweza kucheza katika hatua hii dhidi ya Serena, gwiji wa kweli wa mchezo huu, ni kitu kikubwa.

"Haikuwa rahisi kabisa. Nilijaribu kujiandaa kwa uwezo wangu wote kama navyofanya katika kila mmechi, nilijaribu kutoangalia nani napambana naye. najivunia hasa nilivyopambana na kila kitu."

Andreescu amefikia rekodi ya Monica Seles, ambaye alitwaa ubingwa wa michuano ya Roland Garros mwaka 1990 wakati akishiriki kwa mara ya nne michuano mikubwa, kwa rekodi ya kuwa mchezaji aliyetwaa mapema ubingwa wa michuano mikubwa katika enzi za michuano ya wazi.

Williams, 37, amepata pigo la pili mfululizo katika fainali za Grand Slam katika michuano hiyo iliyofanyika Flushing Meadows, baada ya mwaka 2018 kushindwa na Naomi Osaka, mechi ambayo inakumbukwa kwa jinsi alivyokuwa akimlaumu mwamuzi Carlos Ramos.

"Bianca alicheza mechi kiajabu sana, najivunia kucheza naye na namfurahia. Ilikuwa ni tennis ambayo huwezi kuamini. Kamna yeyote angeweza kushinda hili, mbali na (dada yangu) Venus, nafurahia kwamba ni Bianca," alisema Serena.

Akicheza fainali ya 33 ya Grand Slam, na ya nne tangu acheze kwa mara ya mwisho katika mataji 23 aliyotwaa, Williams alianza mechi hiyom iliyofanyikja uwanja wa Arthur Ashe kwa kupoteza mipira miwili ya mwanzo.

Chanzo: mwananchi.co.tz