Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Naomi amliza Serena Australian Open

29eefab1238ea8d6fd68044b137b9e05 Naomi amliza Serena Australian Open

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERENA Williams jana aliondoka kwenye chumba cha mikutano na waandishi wa habari akibubujikwa machozi baada ya kufungwa na Naomi Osaka kwenye nusu fainali za michuano ya Australian Open.

Gwiji huyo wa Marekani alishuhudia kampeni zake za kubeba taji la 24 la Grand Slam zikifika mwisho kwa kipigo cha 6-3 6-4 kutoka kwa bingwa huyo mara tatu Osaka.

Alipunga mkono wa kwa heri kwa nguvu kwa umati uliokuwa Rod Laver Arena jambo lililoacha maswali juu ya hatima ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39.

Alisema: "Sijui kama ni kusema kwa heri, sitamwambia yeyote.”

Williams aliendelea kububujikwa machozi pale alipoulizwa kuhusu makosa yasiyo la lazima aliyoyafanya dhidi ya Osaka.

"Sijui, nimemaliza," alisema kabla ya kuondoka kwenye chumba cha mkutano.

Williams aliwashukuru mashabiki wake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram muda mfupi baada ya mechi.

"Leo (jana) halikuwa suala la kiwango lakini imetokea, nina furaha kuwa tayari kucheza mbele yenu.”

"Sapoti yenu, upendo wenu, natamani ningefanya vizuri zaidi mbele yenu leo.”

Williams amekuwa akiwania kuweka rekodi tangu aliporejea ulingoni kutoka kwenye uzazi mwaka 2018.

Tangu kurejea kwake kutoka kwenye uzazi, Williams amefuzu fainali nne za Grand Slam lakini alifungwa zote ikiwamo dhidi ya Osaka kwenye US Open 2018.

Ni mara ya kwanza ndani ya miaka 18 kwa Williams kufungwa mechi ya nusu fainali ya Australian Open.

Chanzo: habarileo.co.tz