Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nadal anakaribia kutetea US Open

15338 Pic+nadal TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

New York, Marekani. Dalili za wazi zimeonekana kwa Rafael Nadal kutetea ubingwa wa tenisi wa mashindano ya US Open mwaka huu, baada ya kufika robo fainali.

Nyota huyo kutoka Hispania, anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora, jana alifanya vema kwenye uwanja wa Flushing Meadows, mjini New York, mchezaji kutoka Georgia, Nikoloz Basilashvili.

Hata hivyo Nadal hakupata ushindi kiubwete dhidi ya Basilashvili, anayeshika nafasi ya 37 kwa ubora duniani, kwani ilibidi zichezwe seti nne ndipo apatikane mshindi kwa jumla ya 6-3 6-3 6-7 (6-8) 6-4.

Bahati nzuri kwake ni kuwa katika robo fainali hatacheza na mpinzani wake mkubwa wa ubingwa, Roger Federer, anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani badala yake atachuana na Dominic Thiem raia wa Austria ambaye hayupo ndani ya 20 bora.

Kwa kutinga hatua hiyo inamaanisha kuwa Nadal amefika robo fainali ya mashindano yote makubwa ya Grand Slam mwaka huu, ikiwa ni mara ya kwanza kwake kupata mafanikio makubwa namna hii tangu mwaka 2011.

Nadal alianza kuonyesha dalili za kufanya vema kwenye mashindano ya US Open mwaka huu pale alipotoka nyuma na kumnyamazisha mchezaji aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kufika fainali, Karen Khachanov wa Russia katika raundi ya tatu, licha ya kucheza akiwa na maumivu ya kifundo cha mguu ‘ancle’.

Chanzo: mwananchi.co.tz