Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Muuaji ampa mfadhaiko Serena Williams

12383 Pic+muuaji TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

San Jose, Marekani. Mcheza tenisi mahiri wa Marekani, Serena Williams, amefichua kilichosababisha ang’olewe katika raundi ya kwanza ya mashindano ya Silicon Valley Classic na Johanna Konta.

Serena alisema kuwa alipatwa na mfadhaiko baada ya kumuona mtu aliyemuua kwa kumpiga risasi hadharani dada yake mkubwa, Yetunde Price mwaka 2003, dakika chache kabla ya mchezo huo.

Alisema baada ya kumuona mtu huyo aliyefungwa miaka 15 gerezani kwa kosa la mauaji hayo, moyo wake ulikufa na akili ikamkumbuka hayati dada yake jambo lililomfanya atoke mchezoni bila kutarajia.

Dakika 53 pekee zilitosha kumng’oa Serena na kumfanya Johanna Konta kutinga raundi ya pili ya michuano hiyo akishinda kwa 6-1 6-0 ya mashindano hayo ya Silicon Valley Classic mjini San Jose.

“Sikuwa na nguvu tena katika mchezo ule baada ya kumuona yule muuaji wa dada yangu Yetunde Price, hakika moyo wangu uliumia sana na nguvu zikaniishia,” alisema.

Mishindi huyo wa mataji 23 ya Grand Slam, alisema mapigo ya moyo wake yalikwenda mbio alipomuona Robert Maxfield uwanjani hapo akakumbuka namna walivyopinga Aprili 2006 muuaji huyo alipohukumiwa kwenda jela miaka 15.

“Sijali kwamba kulia kwangu hakuwezi kumrudisha dada yangu kipenzi Yetunde Price, lakini nimeumia na kukumbuka mengi nilikumbuka namna alivyouawa huko Compton, Los Angeles, nikawafikiria watoto wake watatu,” alisema.

Alisema sio haki hata kidogo kwa muuaji kamam huyo kufungwa na baada ya muda anarudi uraiani akiwa huru wakati aliyeuawa harudi tena.

Chanzo: mwananchi.co.tz