Dar es Salaam. Klabu ya Kijitonyama jana ilitawala mashindano ya tenisi yajulikanayo kama ‘BQ Open tennis tournament’ yaliyoanza kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Bq Contractors Limited na Kinywaji cha pepsi yatamalizika leo kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji kutoka klabu za Mkoa wa Morogoro, Arusha, Pwani pamoja na wenyeji Dar es Salaam.
Kijitonyama ilianza kupata ushindi upande vijana wa miaka 12 kwa wavulana baada ya mchezaji wake Adili Nikasi kumshinda Fausal Shabani kwa 4-1,4-2.
Naye Ian Elbariki alimshinda Abdulzaki Kem kwa seti mbili za 4-2,4-0 na Selemani Farid kutoka Gymkhana Dar es Salaam akamshinda Axel Carles wa Kijitonya kwa seti mbili za 4-1,4-3.
Juma Ossi wa Kijitonyama alimshinda Jabir Kessy wa Gymkhana Dar kwa 4-0, 4-2, Mukshin Jabir wa Kijitonyama akamshinda Kennedy Msuva kwa 4-1.4-1.