Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic ajitutumua na kutamba Cincinnati

12218 ATAMBA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Cincinnati, Marekani. Bingwa wa mashindano ya Wimbledon, Novak Djokovic ameweza kuwapa raha mashabiki wake baada ya kumshinda Adrian Mannarino katika mashindano ya Cincinnati.

Djokovic aliyeng’olewa kwenye mashindano ya Rogers Cup wiki iliyopita na Stefanos Tsitsipas wa Ugiriki, katika mchezo wa jana alitoka nyuma na kumshinda Adrian Mannarino na kutinga raundi ya tatu ya Cincinnati Master.

Bingwa huyo anayeshikilia mataji 13 ya Grand Slam, alimshinda Mannarino wa Ufaransa kwa 4-6 6-2 6-1.

Kwa sasa Djokovic, raia wa Serbia anayeshika nafasi ya kumi kwa ubora dunini, atacheza na Grigor Dimitrov wa Bulgeria au Mischa Zverev wa Ujerumani.

Katika mchezo mwingine Marin Cilic wa Croatia alimshinda Marius Copil wa Romania kwa 6-7 (4-7) 6-4 6-4 na Robin Haase wa Uholanzi alimshinda Alexander Zverev wa Ujerumani kwa 5-7 6-4 7-5.

Chanzo: mwananchi.co.tz