Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Croatia yaing’oa Marekani Davis Cup

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zadar, Croatia. Timu ya Taifa ya Croatia 'Dream Team' ya mchezo wa tenisi, jana ilijikatia tiketi ya kucheza fainali ya Davis Cup baada ya kuing’oa Marekani kwa seti 3-2 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mjini Zadar, Croatia.

Shukrani zimemwendee mchezaji wa mwisho wa Croatia kushuka uwanjani, Borna Coric ambaye alimzidi ujanja mpinzani Frances Tiafoe akimshinda kwa seti mbili na kufanya matokeo ya jumla kwa nchi hiyo kuwa 6-7 (0/7), 6-1, 6-7 (11/13), 6-1, 6-3 kuhitimisha ushindi huo.

Kutokana na ushindi huo Croatia itacheza na Ufaransa katika fainali itakayopigwa Novemba mwaka huu ikiwa ni ya tatu katika historia yake, ilicheza fainali yake ya kwanza na kutwaa ubingwa mwaka 2005 kabla ya kucheza tena fainali mwaka 2016 na kufungwa na Argentina.

Mchezo huo wa fainali ya tenisi utakumbushia fainali ya Kombe la Dunia katika mchezo wa soka, uliofanyika Julai mwaka huu na Ufaransa ‘Les Bleus’ kushinda kwa mabao 4-2.

Kocha wa timu ya Taifa ya Croatia, Zeljko Krajan, alimpongeza Coric mwenye miaka 21, kwa kuiwezesha nchi yake kutinga fainali hizo na kuahidi kulitwaa taji hilo.

Ushindi wa Coric uliweza kuufunika kabisa ushidi wa kustusha alioupata Mmarekani Sam Querrey dhidi ya Marin Cilic wa Croatia wa 6-7 (2/7), 7-6 (7/6), 6-3, 6-4.

Chanzo: mwananchi.co.tz