Mchezaji Gofu raia wa Marekani, Brooks Koepka amefanikiwa kutwaa taji la US Open na kumzidi mpinzani wake wa karibu kabisa Tommy Fleetwood na hivyo kutetea ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo.
Koepka mwenye umri wa miaka 28 amefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa maraya pili mfululizo na kuvunja rekodi iliyowekwa na mcheza gofu mwenzake raia wa Marekani, Curtis Strange mwaka 1989 baada ya ushindi wa tofauti ya 68 kwa 63 dhidi ya Fleetwood aliyeshika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Shinnecock Hills Golf Club.
Tano bora kwenye michuano hiyo ya US Open baada ya kumalizika