Bingwa mara mbili wa mashindano ya French Open, Maria Sharapova amelazimika kujiondoa katika mashidano hayo kutokana na majeraha aliyopata.
Sharapova amelazimika kuondolea kwenye mashindano hayo kutoka na matatizo ya bega yanayomkabili.
Mrusi huyo amewahi pia kutwaa taji tuzo ya Gland Slam kwenye halfa iliyofanyika Paris Ufaransa mwaka 2012 na 2014.
Nyota huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akielezea kujitoa kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
Aliandika kwenye Instagram akisema, “Kujitoa kwenye Mashindano ya French Open wakati mwingine kufanya uamuzi kama huo sio jambo rahisi.”
Aliongeza kuwa hata hivyo habari njema amerejea kufanya maozezi mepesi ambayo taratibu yanamuwezesha kuanza kupata ahueni ya maumivu ya kwenye bega linalomsumbua.
Pia Soma
- Simba kuwavaa Mtibwa bila beki benchi
- Dirisha la usajili England kufunguliwa leo, timu vigogo England kusaka kusaka makinda
- Ujio wa Sevilla watikisa maandalizi Simba