Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

walinda milango Ligi Kuu wamuhofia Mayele

Mayele Yanga Fiston Mayele akiwa kashaweka wavuni

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati mashabiki wanachekelea burudani ya mabao ya straika wa Yanga, Fiston Mayele, makipa aliowatunguliwa wamefunguka na kuelezea ujanja alionao staa huyo kusoma alama za nyakati.

Ukiachana na bao alilomfunga Aishi Manula wa Simba kwenye Ngao ya Jamii pale kwa Mkapa, Mayele amezifunga timu zingine nne Ligi Kuu Bara ambazo ni KMC, Azam FC, Mbeya Kwanza na Biashara United na baadhi ya makipa waliokumbana na mashuti yake walielezea namna ambavyo anatumia akili nyingi kujitoa mhanga kwa ajili ya klabu yake.

Kipa wa Mbeya Kwanza, Hamad Kadedi alisema Mayele anafunga mabao ya kuumiza ambayo yamejaa ufundi mwingi na kujitoa mhanga bila kujali kuumia.

“Hakuna kipa ambaye anapenda kufungwa, ila ukisema nizungumzie bao la Mayele alifunga linaloendana na hadhi ya jina lake na klabu anayoichezea, kwa sababu halikuwa rahisi,” alisema.

“Kwanza ni straika ambaye anajua kuutafuta mpira. Nakumbuka bao lile aliwahadaa mabeki kisha akapiga shuti la ufundi. Hilo linatufunza kitu makipa kuwa na mbinu za kukabiliana wachezaji kama Mayele.”

Kipa wa Biashara United, James Setuba alisema ilikuwa vita baina yake na Mayele, kwani alikabiliana naye mara kwa mara hadi alipotumia mbinu kali kumfunga. “Bao la Mayele lilikuwa zuri, kwani lilijaa ufundi zaidi, ingawa ilikuwa ni vita kali baina yake na mimi. Muda mwingi niliiona sura yake mbele yangu. Hata ukimuuliza Mayele atasema namna ambavyo nilikuwa napangua mashuti yake. Ndio kazi natakiwa kuangalia majukumu mengine yaliyopo mbele yangu, kwani ligi ina ushindani mkali,” alisema.

Mayele aliwahi kuzungumzia jina lake la Mayele kwamba ni mtu anayetumia akili na kwamba ndio maana anafunga mabao ya akili. “Kufunga mabao ya akili kwangu siyo ajabu, kwani jina langu la Mayele linamaanisha ni mtu mwenye akili,” alisema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz