Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

neno la mwisho la Morocco kwa Wananchi

Moloko Er neno la mwisho la Morocco kwa Wananchi

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda mchache baada ya kuwekwa wazi kuachwa kwa winga, Jesus Moloko kuachwa na Yanga dirisha hili la usajili kupisha usajili mpya winga huyo amekiri hilo.

Yanga imeachana na winga huyo baada ya kuitumikia kwa misimu miwili hivyo ameungana na Wacongo wenzake Djuma Shaban, Yanick Bangala, Heritier Makambo, Chico Ushindi ambaye hakuweza kuendana na kasi ya Yanga na Fiston Mayele aliyeuzwa nje.

Akizungumza nasi, Moloko alisema ni kweli amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka nchini leo kwenda Congo kwa ajili ya maisha mengine mapya ya soka.

"Ni kweli nimepewa barua ya kuachana na Yanga na natarajia kwenda Congo kesho (leo) nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu hii kwa maisha niliyoishi nao nikiwa ndani ya timu hiyo;

"Nilikuwa na misimu mitatu mizuri na Yanga nimeishi vizuri na wachezaji wenzangu, viongozi na hata mashabiki nawatakia kila la kheri kwenye mashindano wanayoshiriki ndani na nje," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live